- Fadhila ya kuhifadhi Sala ya Alfajiri na Alasiri; Kwa sababu Alfajiri ni wakati wa usingizi mzuri, na Alasiri ni wakati mtu anashughulika na kazi zake, basi atakayezihifadhi atakuwa na haki zaidi ya kuzihifadhi Swala zilizosalia.
- Sala ya Alfajiri na Alasiri zimeitwa baridi mbili; Kwa sababu Swala ya Alfajiri ina ubaridi wa usiku, na Sala ya Alasiri ina ubaridi wa mchana, hata ikiwa ni katika wakati wa joto, ni nyepesi kuliko wakati wa kabla yake, au zimeitwa hivyo kwa kuzingatia kawaida ya nyakati nyingi huwa hivyo, kama ambavyo husemwa: Miezi miwili, kwa kumaanisha jua na mwezi.