- Hatari ya kuchelewa swala ya pamoja msikitini.
- Wanafiki hawakukusudia katika ibada zao isipokuwa kujionyesha na kutaka kusikika, hawaji katika swala ila katika wakati ambao watu wanawaona.
- Malipo makubwa katika swala mbili, Ishaa na Alfajiri kwa jamaa, nakuwa swala hizo zinastahiki zaidi kuziendea hata kwa kutambaa.
- Kuhifadhi swala mbili, Ishaa na Alfajiri ni sababu ya kusalimika na unafiki, na kuto kuzihudhuria ni katika sifa za wanafiki.