Ufafanuzi
Swahaba Abuu Mussa Al-Ash'ary -Radhi za Allah ziwe juu yake- alisali swala moja, alipofika katika kikao cha tahiyatu ambacho kinatashahudi, mtu mmoja akasema miongoni mwa wasaliji walioko nyuma yake: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- alipomaliza swala aliwageukia maamuma, akawauliza: Ni nani kati yenu aliyesema neno: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka?!, Watu wote wakanyamaza, na hakuzungumza yeyote kati yao, akarudia kuwauliza swali mara nyingine, alipoona hakuna alliyemjibu, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- akasema: Huenda ukawa ni wewe Hittwan ndiye uliyesema! Kwa ujasiri wake na ukaribu wake kwake, na mahusiano yake kwake, jambo ambalo haliwezi kupelekea kumtuhumu, na ili ampe msukumo msemaji wa uhakika kukiri, Hittwan akalikanusha hilo, na akasema, nilihofia unaweza kunikaripia kwa kudhani kuwa mimi ndiye niliyesema; na hapa sasa yule bwana akazungumza: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia ila jambo la kheri, Abuu Mussa akasema kwa kumfundisha: Hivi hamjui ni nini mtasema ndani ya swala yenu?! Alisema hivi kwa kukemea kitendo hicho, kisha Abuu Mussa akaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia siku moja, akawabainishia sheria zao, na akawafundisha swala yao, akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-:
Mtakaposali basi nyoosheni safu zenu, na mlingane sawa, kisha mmoja miongoni mwao awasalishe watu, imamu atakapotoa takbira ya kuhirimia swala, basi toeni takbira mfano wake, na akisoma suratul Fatiha na akafikia: "Ghairil magh-dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Fatiha: 7], Semeni: Aaamiin; mkifanya hivyo Mwenyezi Mungu atakujibuni maombi yenu, akitoa takbira na akarukuu basi toeni takbira na mrukuu; kwani imamu anarukuu kabla yenu na ananyanyuka kabla yenu msimtangulie; kwa sababu mahali alipowatangulia imamu ni katika kuwatangulia kurukuu, kutamalizika kwa kuchelewa kwenu kidogo baada ya yeye kunyanyuka kidogo, kitambo hicho kidogo kitapishana kidogo na kunyanyuka kwake, na hapo kiwango cha rukuu yenu kitakuwa sawa na rukuu yake, na imamu akisema: Samiallaahu liman hamidah, basi semeni: Allaahumma Rabbanaa walakal hamdu, waswaliji wakisema hivyo basi hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasikia dua zao na kauli zao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kwa ulimi wa Nabii -Rehema na amani ziwe juu yake-:Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumuhimidi, kisha imamu akitoa takbira na kusujudu basi na maamuma wanatakiwa kutoa takbira na kusujudu, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yao, na anyanyuke kabla yao, kiwango hicho kidogo cha kusubiri kitakuwa sawa na kiwango chake, na hapo kiwango cha maamuma kitakuwa sawa na kiwango cha imamu, ana akifika katika kikao cha tahiyatu, na iwe kauli ya mwanzo ya mwenye kusali ni: "Attahiyyatut twayyibaatu asswalawaatu lillaah" Ufalme na kubakia na utukufu wote unamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, na vile vile swala tano zote ni za Mwenyezi Mungu, "Assalaamu alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh", "Assalaamu alainaa walaa ibaadillaahis swaalihiin, muombe Mwenyezi Mungu akusalimishe na kila aibu na maafa, na mapungufu na maovu; na tunamtaja Muhammadi pekee kwa kumtakia amani, kisha tunajitakia amani wenyewe, kisha tunawatakia amani waja wema wa Mwenyezi Mungu wale wenye kutekeleza haki zilizo juu yao za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waja wake, kisha tunashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na tunashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na Mtume wake.