kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo...
Ameelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kumsikia muadhini kwa ajili ya swala basi naye amfuatilize nyuma yake, aseme mfano wa kauli za...
Kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuh...
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati akimsikia muadhini "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isip...
Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesem...
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati amemsikia muadhini baada ya kumaliza adhana: "Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa wi...
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi...
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, b...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa...
Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi sina wa kunisaidia na kunishika mkon...

kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema, ni kwamba yule atakaye nitakia rehema mara moja Allah atamtakia rehema mara kumi, kisha niombeeni kwa Allah ukaribu, hakika ukaribu huo ni daraja ndani ya Pepo, halipati daraja hilo isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na ninatarajia niwe mimi ndiye huyo mja huyo, na atakayeniombea mimi ukaribu ataupata uombezi".

Kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake".

Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama".

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi sina muongozaji wa kunileta msikitini, akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amruhusu asali nyumbani kwake, akamruhusu, alipoondoka akamuita, akasema: "Je, wasikia wito wa swala?" Akasema: Naam, akasema: "Basi ujibu".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?" Wakasema: Hautobakiza uchafu wowote, akasema: " Huu ndio mfano wa swala tano, Mwenyezi Mungu hufuta makosa kwa swala hizo".

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu" Akasema: Alinihadithia mambo hayo, na lau ningemtaka ziada angenizidishia.

kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku".

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"

Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Ulikuwa usia mkubwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipofikwa na mauti: "(Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume, (Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume", mpaka akaanza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushikwa na kwikwi kifuani kwake kwa maneno hayo kwa sababu ya kifo, na maneno hayo yalikaribia kujaa ulimi wake.

Kutoka kwa Amri Bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nimeigawa swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, na mja wangu ana haki ya kupata alichooomba, atakaposema mja: "Al-hamdulillaahi rabbil aalamiin" (Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu), Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: "Amenihimidi mja wangu", na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim" (Mwingi wa rehema mwenye kurehemu) Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: Kanisifu mja wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin" (Mmiliki wa siku ya malipo) husema: Kanitukuza mja wangu, na mara nyingine husema: Kakabidhi kwangu mja wangu, akisema: "Iyyaaka na'budu wa iyyaaka nastaiin" (Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada) husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu, na mja wangu ana haki ya kupata alichokiomba, akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", husema: Hili ni la mja wangu na mja wangu ana haki ya kupata alichoomba".