Je, wasikia wito wa swala?" Akasema: Naam, akasema: "Basi ujibu
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi sina muongozaji wa kunileta msikitini, akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amruhusu asali nyumbani kwake, akamruhusu, alipoondoka akamuita, akasema: "Je, wasikia wito wa swala?" Akasema: Naam, akasema: "Basi ujibu".
Imepokelewa na Imamu Muslim
Ufafanuzi
Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi sina wa kunisaidia na kunishika mkono kuja msikitini, katika swala tano, akitaka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amruhusu, alipompa mgongo alimuita na akasema: Je, unasikia adhana ya swala? akasema: Ndiyo, akasema: Basi mjibu anayenadi kwa ajili ya swala.
Hadeeth benefits
Uwajibu wa swala ya jamaa; kwa sababu kutaka ruhusa huwa hakuwi ila kwa jambo la lazima.
Kauli yake: "Mjibu" Kwa mwenye kusikia wito inaonyesha kuwa swala ya pamoja ni lazima; kwa sababu asili ya amri ni wajibu.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others