- Ukubwa wa jambo la swala na haki ya mamluki; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliusia mambo hayo mawili katika mwisho wa yale aliyousia.
- Swala ni katika haki kubwa za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kutimiza haki za viumbe na hasa hasa madhaifu, nao ni wale waliochini ya mkono wa mtu wasiokuwa kizazi chake nalo ni katika haki kubwa za viumbe.