- Sheria ya kuomba dua hii baada ya kumaliza kurudia nyuma ya muadhini, na ambaye hatosikia adhana; basi hatakiwi kuisema.
- Ubora wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi kwamba amepewa uwakala na fadhila na nafasi na utetezi mkuu wa kutetea kuhukumiwa baina ya viumbe.
- Kuthibitisha utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa kauli yake: "Ataupata utetezi wangu siku ya Kiyama".
- Utetezi wake rehema na amani ziwe juu yake utakuwa kwa wale waliotenda madhambi makubwa katika umma wake ili wasiingie motoni, au aliyeingia atoke, au katika kuingia peponi pasina hesabu, au kunyanyuliwa daraja aliyeingia.
- Amesema Attwayyibi: kuanzia mwanzo wa "Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu" huu ndio wito uliotimia, na maneno "Hayya a'la" (njooni katika) ndio swala iliyosimama katika kauli yake wanasimamisha swala, na inawezekana kuwa makusudio ya swala hapa ni dua, na kwa mujibu wa hili kauli yake "na swala iliyosimama" ni kubainishwa wito uliyotimia, na inawezekana kuwa makusudio yake ni swala iliyozoeleka wanayoitwa kwayo kwa wakati huo, na ndilo lililokaribu na maana halisi.
- Amesema Al-Mulhab: Katika hadithi hii kuna himizo la kuomba dua katika nyakati za swala; kwa sababu ni hali zinazotarajiwa zaidi kujibiwa dua.