Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haikubali Mwenyezi Mungu...
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa sharti za kusihi swala: Ni twahara, ni wajibu kwa atakayetaka kuswali atawadhe i...
Kutoka kwa Jabiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amenieleza Omari Bin Khattwab: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya ku...
Ameeleza Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuona mtu mmoja kamaliza kutia udhu wake, akaacha...
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Tulirejea tukiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina...
Alisafiri Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina akiwa pamoja na Masahaba zake, wakiwa njiani walipata maji, wakaenda mbio kut...
Kutoka kwa Amri bin Aamiri kutoka kwa Anasi amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala, nikasema: Nyinyi m...
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kwa kila swala ya faradhi hata kama hajatengukwa udhu; Na hii ni kwa sababu ya kupata malipo...
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja.
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja moja, an...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe".
Kutoka kwa Jabiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amenieleza Omari Bin Khattwab: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali.
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Tulirejea tukiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina mpaka tulipofika katika njia yenye maji, walifanya haraka baadhi ya watu kusali laasiri, wakatia udhu wakiwa na haraka, tukawakuta na hali yakuwa visigino vyao vikiwa vyeupe havijaguswa na maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu".
Kutoka kwa Amri bin Aamiri kutoka kwa Anasi amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala, nikasema: Nyinyi mlikuwa mnafanya vipi? Akasema: Ulikuwa ukimtosha mmoja wetu udhu mmoja madam hajatengukwa.
Imepokelewa kutoka kwa Humran kijana wa Othman bin Affan alimuona Othman bin Affan akiomba kuletewa chombo cha udhu, akamimina juu ya mikono yake kutoka katika chombo chake, akaiosha mara tatu, kisha akaingiza mkono wake wa kulia katika chombo, kisha akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga(akayatoa), kisha akaosha uso wake mara tatu, na mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara tatu, kisha akafuta kichwa chake, kisha akaosha kila mguu mara tatu, kisha akasema: Nilimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu wangu huu, na akasema: "Atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili ambazo haizungumzishi ndani yake nafsi yake, basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia".
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke maji puani mwake kisha ayapenge, na atakayestanji kwa mawe basi afanye yawe witiri, na atakapo amka mmoja wenu toka usingizini basi na aoshe mikono yake kabla ya kuingiza ndani ya chombo chake, kwani mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake". Na lafudhi ya Muslim: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini kwake basi asizamishe mkono wake ndani ya chombo mpaka auoshe mara tatu, kwani hajui ni wapi ulilala mkono wake".
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".
Imepokewa Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.