- Swala ya mtu mwenye hadathi (kama janaba, hedhi au nifasi) haikubaliki mpaka ajitwaharishe kwa kuoga kutokana na hadathi kubwa, na kwa kutawadha ikiwa ni hadathi ndogo (kama kwenda haja kubwa au ndogo, au kulala, au kutokwa upepo)
- Udhu ni kuchukua maji na kuyazungusha mdomoni na kuyatoa, kisha kuvuta maji kwa pumzi mpaka ndani ya pua, kisha kuyatoa na kuyapenga, kisha mtu ataosha uso wake mara tatu, kisha ataosha mikono yake pamoja viwiko viwili mara tatu, kisha atafuta kichwa chake mara moja, kisha kuosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu.