- Ulazima wa kuosha miguu miwili katika udhu; kwa sababu lau kama ingefaa kufuta asingetoa ahadi ya adhabu ya moto kwa mwenye kuacha kuosha mwisho wa miguu yake.
- Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vyenye kuoshwa wakati wa udhu, nakuwa atakayeacha sehemu ndogo ambayo ni ya wajibu kusafishwa kwa makusudi au kwa uzembe, basi swala yake haisihi.
- Umuhimu wa kumfundisha asiyejuwa na kumuelekeza.
- Msomi anatakiwa kukemea anayoyaona ikiwemo kupoteza wajibu na sunna, lakini kwa usulubu mzuri.
- Amesema Muhammad Is-haqa Al-Dahalawi: Kueneza maji kuna aina tatu: Lazima (Faradhi) Nako ni kueneza maji mahali unapoosha kwa mara moja, na sunna: Nayo nikuosha kiungo mara tatu, na inapendeza:
- kurefusha mahali unapoosha ikiwa ni pamoja na kufanya hivyo mara tatu.