Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili
Kutoka kwa Abdallah bin Zubairi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Ufafanuzi
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara mbili, anaosha uso ikiwemo kusukutua na kupandisha maji puani na mikono miwili na miguu miwili mara mbili.
Hadeeth benefits
Kilicho wajibu katika kuosha viungo ni mara moja moja na kinachozidi inapendeza.
Sheria ya kutia udhu mara mbili mbili katika baadhi ya nyakati.
Sheria katika kufuta kichwa ni mara moja.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others