Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala
Kutoka kwa Amri bin Aamiri kutoka kwa Anasi amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala, nikasema: Nyinyi mlikuwa mnafanya vipi? Akasema: Ulikuwa ukimtosha mmoja wetu udhu mmoja madam hajatengukwa.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Ufafanuzi
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kwa kila swala ya faradhi hata kama hajatengukwa udhu; Na hii ni kwa sababu ya kupata malipo na fadhila.
Na inafaa kwa mtu kuswali kwa zaidi ya swala moja kwa udhu mmoja madam bado yuko na udhu wake.
Hadeeth benefits
Mwenendo uliodumu zaidi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kushika udhu kwa kila swala; ili kutaka ukamilifu zaidi.
Sunna ya kushika udhu kila wakati wa swala.
Inafaa kutekeleza zaidi ya swala moja kwa udhu mmoja.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others