- Inapendeza kuosha mikono miwili kabla ya kuiingiza katika chombo mwanzo wa udhu, hata kama hajaamka kutoka usingizini, na akiwa kaamka kutoka usingizini basi ni wajibu kuiosha.
- Ni lazima mwalimu atumie njia ya karibu na uelewa na kuifanya elimu ikite kwa mwenye kujifunza, na katika hilo ni kufundisha kwa vitendo.
- Ni lazima kwa mwenye kuswali kuzuia mawazo yanayohusiana na shughuli za kidunia, utimilifu wa swala na ukamilifu wake ni katika kuhudhuria moyo ndani yake, na kama si hivyo mawazo ni vigumu kusalimika nayo, anatakiwa apambane na nafsi yake na asiruhusu yaendelee.
- Sunna ya kuanza na kulia katika udhu.
- Sheria ya kupangilia kati ya kusukutua na kupandisha maji puani na kupenga.
- Sunna ya kuosha uso na mikono miwili na miguu miwili mara tatu tatu, na wajibu ni mara moja.
- Mwenyezi Mungu kuyasamehe yaliyotangulia katika madhambi kunaambatana na mambo mawili: Udhu, na kuswali rakaa mbili, kwa sifa iliyotajwa katika hadithi.
- Kila kiungo katika viungo vya udhu kina mpaka: Mpaka wa uso: Kwa urefu ni kuanzia maoteo ya nywele za kichwa ya kawaida, mpaka chini katika ndevu na kidevu, na kwa upana ni sikio kwa sikio. Na mpaka wa mkono: Ni kuanzia ncha za vidole mpaka katika kiwiko nayo ni maungio kati ya muhundi na sehemu ya juu kuelekea begani. Na mpaka wa kichwa: Ni kuanzia maoteo ya kichwa ya kawaida kando kando ya uso mpaka juu ya shingo, na kufuta masikio mawili ni sehemu ya kichwa. Na mpaka wa mguu ni: Mguu wote pamoja na maungio kati yake na muhundi.