Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa ms...
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara nyingi akipiga mswaki na akiamrisha watu kufanya hivyo, na kuna baadhi ya nyakati kumetiliwa mkazo,...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti nisingeliogopea uz...
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake lau kama si hofu ya kuwatia tabu waumini katika umma wake basi angeliwawajibishia juu yao kutumia mswaki...
Na imepokelewa katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ni haki kwa kila muislamu aoge k...
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni haki iliyotiwa mkazo kwa kila muislamu aliyebalehe mwenye akili timamu aoge katika kila siku saba z...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya...
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo matano katika dini ya Uislamu na sunna ya Mitume: La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi...
Imepokewa Kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliz...
Ameeleza Ally bin Abiy Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye ilikuwa mara nyingi akitokwa na madhii -nayo ni maji meupe mepesi yenye utelezi...

Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala".

Na imepokelewa katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".

Imepokewa Kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe" Na katika sahihi Bukhari: Akasema: "Tawadha na uoshe tupu yako".

Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga, kisha anaachanisha nywele zake kwa mkono wake, mpaka pale anapohisi kuwa ngozi yake yote imeenea maji, anajimwagia maji kwa michoto mitatu, kisha anaosha mwili wake wote uliobakia, na Aisha akasema: Nilikuwa nikioga mimi na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja, tukichota sote katika chombo hicho.

Kutoka kwa Ammari Bin Yasiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliniagiza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika haja fulani, nikapatwa na janaba, nikawa sikupata maji, nikajigaragaza katika udongo kama anavyojigaragaza mnyama, kisha nikamuendea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Nikamsimulia hilo, akasema: "Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hivi" Kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha ukapaka mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake".

Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Mimi hupatwa na hedhi ya ugonjwa na sitwahariki, je niache swala? Akasema: "Hapana, hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba".

Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu, akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu. kisha akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, Akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, kisha akasema: Hayya ala Swalaah, akasema: Laa Haula wala Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Hayya ala lfalaah, akasema: Laa Haula walaa Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Laa ilaha ila llahu, akasema: Laa ilaha ila llahu, kutoka ndani ya moyo wake, basi ataingia peponi".