- Josho lina aina mbili: Linalotosheleza na lilokuwa kamili, ama josho linalotosheleza ni mtu kunuia twahara, kisha akaeneza maji katika mwili wake ikiwa ni pamoja na kupandisha maji puani na kusukutua, na ama josho lilokuwa kuwa kamili ataoga kama alivyo oga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithi hii.
- Neno Janaba hutumika kwa kila aliyetoa manii, au kafanya tendo la ndoa hata kama hajamtoka.
- Inaruhusiwa mwanandoa kutazama uchi wa mwenzake, na kuoga pamoja katika chombo kimoja.