- Ubora wa Ally bin Abi Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi ambacho haya haikumzuia kuacha kuuliza kupitia mtu mwingine.
- Inafaa kutuma mtu kwa niaba kwa ajili ya kuuliza.
- Inafaa kumueleza mtu mambo binafsi kwa sababu ya kuona haya ikiwa kuna masilahi.
- Unajisi wa madhii, na uwajibu wa kuyaosha katika mwili na nguo.
- Kutoka kwa madhii ni katika vitenguzi vya udhu.
- Uwajibu wa kuosha utupu na korodani mbili kwa kuwa zimetajwa katika hadithi nyingine.