- Kutilia umuhimu na kujali kwa Uislamu swala la usafi na twahara.
- Kuoga siku ya Ijumaa kumependekezwa sana tena kwa mkazo kwa ajili ya swala.
- Kimetajwa kichwa, pamoja nakuwa kutajwa mwili kungetosha kukusanya na kichwa; Lakini ni kwa ajili ya kukitilia maanani.
- Ni wajibu kuoga kwa kila aliyepatwa na harufu mbaya, inayo waudhi watu.
- Siku muhimu zaidi kwa ajili ya kuoga ni siku ya Ijumaa; kwa sababu ya fadhila zake.