- Mkazo wa sheria ya kupiga mswaki baada ya usingizi wa usiku, kwa sababu usingizi hupelekea mabadiliko ya harufu ya kinywa, na mswaki ndio kifaa cha kusafishia.
- Mkazo wa sheria ya kupiga mswaki kila wakati wa mabadiliko ya harufu ya kinywa, kwa kuzingatia maana ya awali.
- Sheria ya usafi kwa ujumla, na kwamba ni sehemu ya Sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ni katika adabu tukufu.
- Kupiga mswaki katika kinywa chote kunajumuisha: Meno, fizi, na ulimi.
- Mswaki ni kijiti kilichokatwa kutoka katika mti wa araki au mti mwingine, na hutumika kusafisha kinywa na meno, na huburudisha kinywa, na kuondoa harufu mbaya.