- Sheria ya kufuta juu ya khufu mbili inakuwa wakati wa kutia udhu kwa ajili ya hadathi ndogo, ama kuoga kwa ajili ya hadathi kubwa ni lazima kuosha miguu.
- Kufuta kunakuwa mara moja kwa kupitisha mkono ulioloana juu ya khufu nasi chini yake.
- Ni sharti wakati wa kufuta juu ya khufu iwe kuzivaa kwake ni baada ya udhu kamili ambao aliosha miguu yake wakati huo kwa maji, na khufu ziwe twahara (safi) na zifunike mahali panapolazimika kuoshwa katika miguu, na kuwe kufuta ni katika hadathi ndogo si katika janaba au chochote kinachowajibisha kuoga, na kufuta kuwe katika muda uliopangwa kisheria nao ni usiku na mchana kwa mwenyeji na siku tatu kwa msafiri.
- Kitapimwa katika khufu mbili kila chenye kusitiri miguu miwili kama soksi na kinginecho, inafaa kufuta juu yake.
- Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mafundisho yake, kiasi kwamba alimzuia Mughira kumvua, na akamueleza sababu: Kuwa alizivaa akiwa twahara; ili nafsi yake itulizane, na ajue hukumu ya hilo.