- Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, na ni kanuni miongoni mwa kanuni za kisheria, nayo ni; Yakini haiondoki kwa shaka, na asili ni kubaki hali iliyokuwa kama ilivyokuwa, mpaka mtu apate uhakika wa kinyume chake.
- Shaka haiathiri katika twahara, na mswaliji ataendelea kubaki katika twahara yake madama hajapata uhakika wa hadathi (kutengukwa udhu).