- Sunna za Mitume anazozipenda Mwenyezi Mungu na kuziridhia na anaziamrisha, zinapelekea katika ukamilifu na usafi na uzuri.
- Sheria ya kushikamana na mambo haya, na kutoghafilika nayo.
- Mambo haya yanafaida za kidini na kidunia, miongoni mwake: Kupendezesha muonekanao, na kusafisha mwili, na kujiweka tayari kwa usafi, na kwenda kinyume na makafiri, na kutekeleza amri ya Allah.
- Kumetajwa katika hadithi zingine ziada ya jambo jingine la kimaumbile tofauti na matano haya, mfano: Kufuga ndevu, na mswaki na nyinginezo.