- Mate ya mbwa ni najisi tena ni najisi nzito.
- Mbwa kulamba katika chombo, kunakitia najisi chombo hicho, na kunanajisisha maji yaliyoko ndani yake.
- Kusafisha kwa udongo na kurudia mara saba hii ni maalum kwa kusafisha pale atakapo lamba, lakini si katika mkojo wake na uchafu wake na vyote atakavyovichafua mbwa.
- Jinsi ya kuosha chombo kwa udongo: Ataweka maji ndani ya chombo na kuongeza udongo ndani yake, kisha atasafisha chombo kwa mchanganyiko huu.
- Maana ya dhahiri ya Hadith ni kuwa hadithi hii inajumuisha mbwa wote, hata mbwa ambao sheria imeruhusu kufugwa, kama vile kuwinda, kulinda, na mbwa wa mifugo.
- Sabuni na majani ya miti havichukui nafasi ya udongo; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliweka sharti la kutumia udongo.