- Uwajibu wa kuoga kwa mwanamke zinapomalizika siku za hedhi yake.
- Uwajibu wa kuswali kwa mwenye istihadha (Hedhi ya ugonjwa).
- Hedhi: Ni damu ya maumbile ambayo hutolewa na mfuko wa uzazi kupitia tupu ya mwanamke aliyevunja ungo, humpata katika siku maalum.
- Istihadha: Ni kutiririka kwa damu nje ya wakati wake kutoka nje ya mfuko wa uzazi na si ndani yake.
- Tofauti kati ya istihadha na damu ya hedhi: Nikuwa damu ya hedhi ni nyeusi nzito inaharufu mbaya, ama damu ya istihadha ni nyekundu nyepesi na haina harufu mbaya.