- Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa umma wake, na kuchelea kwake kuwatia tabu juu yao.
- Asili katika amri za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni ulazima, isipokuwa itakapokuja dalili kuwa ni sunna.
- Sunna ya kupiga mswaki na fadhila zake wakati wa kila swala.
- Amesema bin Daqiq Al-Idd: Hekima ya kufanywa sunna ya mswaki wakati wa kusimama katika swala ni kwa sababu ni mtu ajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, ikawa ni lazima awe katika hali ya ukamilifu na usafi na kuonyesha heshima ya ibada.
- Ujumla wa hadithi unajumuisha kupiga mswaki kwa mfungaji hata ikiwa baada ya kupinduka jua, kama swala mbili za Adhuhuri na Lasiri.