- Swala inayofuta madhambi ni ile ambayo mja katawadha vizuri udhu wake, na akaitekeleza kwa unyenyekevu akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa swala hiyo.
- Fadhila za kudumu katika ibada, nakuwa ibada ni sababu ya kusamehewa madhambi madogo.
- Fadhila za kutawadha vizuri, na kuswali vizuri pamoja na utulivu ndani yake.
- Umuhimu wa kuyaepuka madhambi makubwa ili kusamehewa madhambi madogo.
- Madhambi makubwa hayafutwi ila kwa toba.