- Kuzidiana kwa amali kati yake ni kulingana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa amali hiyo.
- Himizo kwa muislamu katika kupupia amali bora kisha inayofuata kwa ubora.
- Kutofautiana kwa majibu ya Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhusu amali bora kulingana na watu na hali zao, na kulingana na lenye manufaa mengi kwa kila mmoja miongoni mwao.