- Himizo la kumjibu muadhini.
- Fadhila za kumtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumjibu muadhini.
- Himizo la kumuombea ukaribu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumtakia rehema.
- Kumebainishwa maana ya ukaribu, na ukubwa wa nafasi yake, kiasi kwamba haumstahiki ila mja mmoja pekee.
- Kumebainishwa ubora wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi ambacho kapendelewa nafasi hiyo ya juu.
- Atakayemuomba Mwenyezi Mungu ukaribu kwa ajili ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi atastahiki kupata uombezi.
- Kumebainishwa unyenyekevu wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba ameuomba umma wake umuombee dua ili apate nafasi hiyo, pamoja nakuwa nafasi hiyo itakuwa yake.
- Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake, jema moja linalipwa kwa mema kumi mfano wake.