Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila...
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema baada ya kumalizika kwa swala za faradhi: Mara thelathini na tatu (33): (Sub-haanalla...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila swala mara thelathini na tatu (33), na akamhimidi Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu (33), na akamtukuza Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, hizo ni tisini na tisa (99) Na akasema ili kukamilisha mia moja (100): Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul hamdu, wahuwaa'laa kulli shai in qadiir, basi yatasamehewa madhambi yake, hata kama yalikuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".

Kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa".

Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema : Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri.

Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kati ya kila adhana mbili kuna swala, kati ya kila adhana mbili kuna swala" Kisha akasema katika mara ya tatu: "Kwa atakayetaka"

Kutoka kwa Abuu Qatada As-sulami Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla hajakaa".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo".

Kutoka kwa Imran bin Huswain -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Niliugua bawasiri, nikamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kusali, akasema: "Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi swali ukiwa umekaa, usipoweza basi ukiwa umelala ubavu".

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazo swaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka".

Kutoka kwa Mahmud bin Labidi radhi za Allah ziwe juu yake: Anasimulia kuwa Othman bin Affan alitaka kujenga msikiti watu hawakulipenda swala hilo, na wakapendelea auache katika muonekano wake, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayejenga msikiti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atamjengea Peponi nyumba mfano wake".

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni, basi litachemshwa katika moto wa Jahanam, kisha zitapigwa pasi mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila linapopoa linarejeshewa umoto, katika siku ambayo makadirio yake yatakuwa ni miaka elfu hamsini, (atadumu katika adhabu hiyo) mpaka watu watakapohukumiwa, naye akaona njia yake, ima inakwenda peponi, na ima anakwenda motoni"

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Sadaka haikuwahi kupunguza chochote katika mali, na hakuna jambo zuri zaidi analomzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa kusamehe zaidi kama kupewa utukufu, na hakuwahi kunyenyekea yeyote kwa ajili Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua".