Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi swali ukiwa umekaa, usipoweza basi ukiwa umelala ubavu
Kutoka kwa Imran bin Huswain -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Niliugua bawasiri, nikamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kusali, akasema: "Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi swali ukiwa umekaa, usipoweza basi ukiwa umelala ubavu".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Ufafanuzi
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa asili katika swala ni kusali kwa kusimama, isipokuwa katika hali ya kutoweza hapo mtu atasali kwa kukaa, na ikiwa hatoweza kukaa atasali kwa ubavu.
Hadeeth benefits
Swala haidondoki kwa muda ambao akili bado ipo, itakuwa kwa kuhama kutoka hali moja kwenda nyingine kadiri ya uwezo.
Huruma na wepesi wa Uislamu kwa kumpa uhuru mja afanye kadiri awezavyo katika ibada.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others