Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazo swaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazo swaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka".
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Ufafanuzi
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuswalia katika msikiti wake, nakuwa ni thawabu bora kuliko swala elfu moja (1000) katika misikiti mingine katika misiti ya ardhini, isipokuwa msikiti mtukufu wa Makka, huo ni bora kuliko swala ya msikiti wake rehema na amani ziwe juu yake.
Hadeeth benefits
Kuzidishwa kwa malipo ya swala katika msikiti mtukufu (wa Makka), na msikiti wa Mtume.
Swala katika msikiti mtukufu wa Makka ni bora kuliko swala laki moja (100,000) katika misiki mingine.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others