- Sunna ya dhikiri hizi kuzisema baada ya swala za faradhi.
- Dhikiri hizi ni sababu ya kusamehewa madhambi.
- Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehema zake na msamaha wake.
- Dhikiri hii ni sababu ya kusamehewa madhambi, na kinachokusudiwa hapa ni: kufutiwa madhambi madogo, ama madhambi makubwa hakuna kinachoweza kuyafuta isipokuwa toba.