- Uharamu wa mazungumzo wakati wa hotuba, hata kama ni kuzia uovu au kujibu salamu au kumuombea dua aliyepiga chafya.
- Anaondolewa katika katazo hili atayemsemesha imamu au imamu akamsemesha yeye.
- Inafaa kuzungumza kati ya hotuba mbili.
- Akitajwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na imamu akiwa katika hotuba basi unatakiwa kumswalia kwa siri, na hivyo hivyo kuitikia dua.