Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayefunga Ramadhani kwa i...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayefunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, na kwa kuitakidi ulazima wa swaumu n...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milang...
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa unapoingia mwezi wa Ramadhani hutokea mambo matatu: La kwanza: Hufunguliwa milango ya pepo na haufun...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au...
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekula au kunywa kwa kusahau akiwa kafunga swaumu ya faradhi au sunna basi atimize swaumu ya...
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yak...
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alidumu na itikafu katika siku kumi za mwisho...
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za...
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake zinapokuja siku kumi za mwisho wa ramadhani anajitahidi ndani yake kwa kufanya ibada na utiifu, na akipiti...

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayefunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo toka kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia"

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha".

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu siku kumi za mwisho wa Ramadhani, mpaka alimpomfisha Mwenyezi Mungu, kisha wakakaa itikafu wake zake baada yake.

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhani) anauhuisha usiku, na anawaamsha watu wake, na anaongeza juhudi na anakaza kikoi".

Imepokelewa na Abii Said Al-khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala".

Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka".

Kutoka kwa Abuu Ubaidi, mwachwa huru wa bin Azhari, amesema: Nilishuhudia swala ya Idd pamoja na Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Siku mbili hizi alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga ndani yake: Siku ya kufungua kwenu kutoka katika swaumu yenu, na siku nyingine ni ile mnayokula katika vichinjwa vyenu.

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia."

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"