- Amesema Nawawi: Fadhila za kufunga katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hili linachukuliwa kwa yule ambaye hadhuriki kwa swaumu hiyo, na wala hapotezi haki zake, na wala hatopoteza mapambano yake wala kinginecho katika majukumu mapigano yake.
- Himizo na hamasisho la kufunga swaumu ya hiyari.
- Uwajibu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala asifunge kwa kujionyesha wala kutaka kusikika, wala kwa makusudio mengine.
- Amesema As-sanadi: Kauli yake "Katika njia ya Mwenyezi Mungu", inategemea kuwa masukudio yake ni nia pekee, na inawezekana kuwa makusudio yake nikuwa amefunga akiwa katika hali ya vitani, na la pili ndio liko karibu na usawa.
- Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Viangazi sabini" Kiangazi ni wakati maalumu wa mwaka, na makusudio yake hapa ni mwaka, na kutajwa kiangazi pekee hapa pasina kutaja wakati uliobakia -kama kiangazi na masika, na kipupwe-; kwa sababu kiangazi ndio kipindi kizuri zaidi kwani hua ndio muda wa kuvuna matunda.