- Fadhila za mwezi wa Ramadhani.
- Habari njema kwa wafungaji ndani yake kuwa mwezi huu mtukufu ni msimu wa ibada na kheri.
- Katika kufungwa mashetani ndani ya Ramadhani ni ishara ya kuondolewa udhuru kwa kila aliyelazimishwa kutekeleza sheria na ni kana kwamba anamwambia:
- Amesema Al-Qurtubi: Ikiwa patasemwa: Inakuwaje tunaona shari na maasi yanatokea ndani ya Ramadhani kwa wingi, na kama mashetani yangefungwa basi tusingeona? Jawabu: Ni kuwa maasi hupungua kwa wafungaji swaumu ambayo zimehifadhiwa sharti zake na zikazingatiwa adabu zake, au nikuwa wanaofungwa ni baadhi ya mashetani nao ni wale wakaidi na si wote kama ilivyotangulia katika baadhi ya riwaya, au makusudio yake ni kupungua kwa shari ndani yake, na jambo hili linaonekana, kwani kutokea kwake ni mara chache kuliko miezi mingine, kwani si lazima kufungwa wote kuwa kusitokee shari wala maasi; kwa sababu hilo lina sababu zingine zisizokuwa mashetani kama nafsi chafu na mazoea mabaya na mashetani wa kibinadamu.