- Kukubalika kwa swaumu ya aliyekula au kunywa kwa kusahau.
- Hana dhambi aliyesahau akala au kunywa; kwa sababu hilo si kwa maamuzi yake.
- Upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwafanyia wepesi juu yao na kuwaondolea tabu na uzito juu yao.
- Hafungui mfungaji kwa chochote katika vile vyenye kufunguza ila zikikamilika sharti tatu: Ya kwanza: Awe anajua, akiwa mjinga hafungui, ya pili: Awe na kumbukumbu, kama kasahau swaumu yake ni sahihi na wala halazimiki kulipa, ya tatu: Iwe kwa hiari yake, na si kwa kulazimishwa, yaani atumie vyenye kufunguza kwa hiari yake mwenyewe.