- Sheria ya kukaa itikafu misikitini, hata kwa wanawake kwa kuzingatia vigezo vya kisheria, na kwa sharti la kuwa na amani dhidi ya fitina.
- Inakuwa na mkazo itikafu katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani kwa kudumu nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Itikafu ni sunna endelevu wala haikufutwa, kwani walikaa itikafu wake zake Mtume rehema na amani ziwe juu yake baada yake.