- Sunna ya kula daku na kutekeleza amri ya sheria kwa kufanya hivyo.
- Amesema bin Hajari katika kitabu Fat-hulbaari: Baraka katika daku zinapatikana kwa namna nyingi: Nayo ni kufuata sunna na kwenda kinyume na Mayahudi na Wakristo, na kupata nguvu kutokana na daku kwa ajili ya ibada, na kuongeza uchangamfu, na kuondoa tabia mbaya inayosababishwa na njaa, na kuwa sababu ya kutoa sadaka kwa mwenye kuomba kwa wakati huo, au akajumuika pamoja naye katika chakula, na ni sababu ya kufanya dhikri na dua katika wakati ambao kuna matarajio makubwa ya kujibiwa, na kuipata nia ya kufunga kwa yule aliyejisahau kabla ya kulala.
- Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa akioanisha hukumu kwa hukumu; ili mioyo ya watu ikunjuke, na ujulikane utukufu wa sheria.
- Amesema bin Hajari: Daku inapatikana kwa chochote kidogo atakachokula mtu, katika vyakula au vinywaji.