Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anawachukia miongoni mwa watu mwenye ugomvi mkali na mw...
Imepokewa Kutoka kwa Abii Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Wakikutana waislamu...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, akiwa na dhamira kila mmoja wao ya kummaliza mwenzake;...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubeb...
Anamtahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeyote atakayebeba silaha dhidi ya waislamu, kwa ajili ya kuwatisha au kuwapora, atakayefanya h...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- uharamu wa kuwatukana wafu na kuchafua heshima zao, nakuwa hili ni katika tabia mbaya, kwani wao wam...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu...
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu kumhama ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote hamsalimii wala hamsemeshi....
Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".
Imepokewa Kutoka kwa Abii Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu huyu muuaji anaeleweka, na vipi kuhusu muuliwaji? Akasema: "Hata yeye alikuwa na pupa ya kumuuwa mwenzake".
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu".
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".
Imepokelewa Kutoka kwa Sahal Ibn Sa'd -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo".
Kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa kapigana vita pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- takriban vita kumi na mbili (12) anasema: Nilisikia mambo manne kutoka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, yakanifurahisha sana, anasema: "Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake (Ndugu asiyeweza kumuoa), hakuna kufunga ndani ya siku mbili: Idil Fitri na Idil Adh-ha, na hakuna swala baada swala ya Asubuhi mpaka lichomoze jua, na wala baada ya Lasiri mpaka lizame, na wala haifungwi safari isipokuwa katika misikiti mitatu: Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Aqswa (Palestina), na msikiti wangu huu (Madina)".
Kutoka kwa Osama bin Zaidi -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Sikuacha baada yangu fitina yenye madhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake".
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio".
imepokewaKutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake"
Kutoka kwa Muawia Al-Qushairi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akasema: "Ni umlishe pale unapokula, na umvishe unapovaa, au utakapopata kipato, na wala usipige uso, na wala usitoe maneno machafu, na wala usihame isipokuwa ndani ya nyumba".
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema: "Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".