- Hadithi ni ushahidi wa uharamu wa kuwatukana wafu.
- Kuacha kuwatukana wafu kuna kuchunga masilahi ya waliohai, na kuhifadhi amani ya jamii kutokana na kutotiliana vinyongo na chuki.
- Hekima ya kukatazwa kuwatukana nikuwa tayari wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza, kuwatukana hakusaidii, na kuna kuwaudhi ndugu zake wa karibu.
- Nikuwa haifai kwa mwanadamu kusema maneno yasiyo na manufaa.