- Sunna kwa wanawake kutoka kwenda katika swala ya Iddi, na watengewe muda wa mawaidha.
- Kuwapinga waume na kukithirisha laana ni katika madhambi makubwa; kwa sababu kuahidiwa moto ni katika alama za dhambi kuwa katika madhambi makubwa.
- Hapa kumebainishwa kuzidi kwa imani na kupungua kwake, yatakayekithiri matendo yake, basi imani yake na dini yake vitazidi, na zitakayepungua ibada zake dini yake itapungua.
- Amesema Imam Nawawi: Akili inakubali kuzidi na kupungua, na vile vile imani, na si makusudio ya kutajwa mapungufu kwa wanawake ni kuwalaumu kwa hilo; kwa sababu hilo ni katika asili ya maumbile, lakini tanbihi katika hilo ni kutahadharisha kutofitinika nao, na ndio maana amepanga adhabu kwa yale yaliyotajwa ikiwemo kuwapinga waume na mengineyo na si katika mapungufu, na mapungufu ya dini hayaishii tu katika madhambi bali ni zaidi ya hayo.
- Hapa kuna swala la mwanafunzi kumrejea mwalimu, na mfuasi kumrejea anayemfuata katika yale ambayo kwake maana haijawa wazi.
- Ndani ya hadithi kumeelezwa kuwa ushahidi wa mwanamke mmoja ni nusu ya ushahidi wa mwanaume mmoja, na hii ni kwa sababu ya upungufu wa kumbukumbu zake.
- Amesema bin Hajari katika kauli yake: "Sijapata kuona wapungufu...mpaka mwisho" Kinachodhihiri kwangu nikuwa, hili ni miongoni mwa sababu za kuwa kwao wengi motoni; kwa sababu wao wakiwa sababu ya kuondoa akili ya mwanaume shupavu mpaka akafikia kufanya au kusema maneno yasiyofaa watakuwa wameshirikiana naye katika madhambi na tena wamemzidi.
- Uharamu wa swala na swaumu kwa mwanamke wakati wa hedhi yake, na mfano huo huo kwa mwenye nifasi, kisha watalipa swaumu pekee watakapokuwa twahara.
- Uzuri wa tabia ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani aliwajibu wanawake maswali yao pasina ukali wala kuwalaumu.
- Amesema bin Hajari: Nikuwa sadaka inazuia adhabu, nakuwa inafuta makosa yaliyoko baina ya viumbe.
- Amesema Nawawi: Upungufu wa dini kwa wanawake kwa sababu ya kuacha kwao swala na swaumu katika wakati wa hedhi; kwa sababu zitakayekithiri ibada zake basi itaongezeka imani yake na dini yake, na zitakayepungua ibada zake itapungua dini yake, kisha upungufu wa dini unaweza kuwa katika sura ambayo anapata dhambi, kama atakayeacha swala au swaumu au mengineyo katika ibada za wajibu juu yake pasina udhuru, na inaweza kuwa katika sura ambayo hapati madhambi, kama atakayeacha swala ya Ijumaa au kwenda vitani au mengineyo ambayo si wajibu juu yake pasina udhuru, na inaweza kuwa katika sura ambayo yeye ndiye kalazimishwa kwa hilo, kama mwenye hedhi kuacha swala na swaumu.