Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo
Imepokelewa Kutoka kwa Sahal Ibn Sa'd -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili nayo muislamu basi ataingia Peponi,
La kwanza: Kuhifadhi ulimi kutozungumza yale yenye kumchukiza Allah Mtukufu,
La pili: Kuhifadhi tupu kutotumbukia katika machafu;
Kwa sababu viungo viwili hivi hukithiri kutokea maasi kwavyo.
Hadeeth benefits
Kuhifadhi ulimi na tupu ni njia ya kuingia Peponi.
Umetajwa mahususi ulimi na utupu; kwa sababu ndio vyanzo vikuu vya balaa kwa mwanadamu katika dunia na Akhera.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others