- Anastahiki adhabu mwenye kukusudia madhambi kwa moyo wake na akazifanya sababu zake.
- Tahadhari kali ya kutopigana waislamu kwa waislamu, na kuna ahadi ya moto.
- Mapigano kati ya waislam kwa haki hayaingii katika ahadi hii ya adhabu, mfano kama kuwapiga vita waasi na mafisadi.
- Mwenye kutenda dhambi kubwa hakufuru kwa kulifanya pekee; Kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kawaita wenye kupigana kuwa ni waislamu.
- Watakapokutana waislamu wawili kwa nyenzo yoyote miongoni mwa nyenzo za kuuwana, mmoja akamuunza mwenzake, basi muuwaji na muuliwaji wote motoni, na kutajwa panga katika hadithi ni sehemu ya mfano tu.