- Himizo la kushikamana na uchamungu, na kutojishughulisha na mambo ya kidunia na pambo lake.
- Tahadhari ya kufitinika na wanawake, kwa kuwatazama au kujiachia kwa kuchanganyika na wanaume wa kando, au mengineyo.
- Fitina ya wanawake ni katika fitina kubwa katika Dunia.
- Kuzingatia na kuchukua mafunzo kutoka katika umma zilizotangulia, kilichotokea kwa wana wa Israeli kinaweza kutokea kwa wengine pia.
- Fitina ya wanawake, akiwa ni mke anaweza kumbebesha mwanaume mzigo mkubwa wa matumizi asiouweza, na akamshughulisha na kutafuta mambo ya kidunia, na akampelekea kumaliza umri wake katika kuitafuta Dunia, na akiwa ni mwanamke wa kando, anaweza kumfitini kwa kumlaghai mwanaume na kumtoa katika haki pale wanawake wakitoka na kuchanganyika pamoja na wanaume, hasa hasa wakiwa hawajisitiri kisheria, na hili linaweza kupelekea kuingia katika zinaa kwa ngazi zake, hivyo ni lazima kwa muumini kujikinga kwa Mwenyezi Mungu, na kuelekea kwake ili kusalimika na fitina za zao.