Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Tahadharini sana na kui...
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala la kuchanganyikana na wanawake wa kando, na akasema: Jiepusheni sana kuingia kwa wanawake, n...
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msi...
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwanamke haikubaliki ndoa yake ila kwa walii atakayesimamia kufungwa kwa ndoa.
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya w...
Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanamke kujiozesha mwenyewe pasina idhini ya walii wake, nakwamba ndoa yake ni batili, na hilo al...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amelaaniwa mwenye kumuing...
Anamtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume kumuingilia mkewe katika utupu wake wa nyuma; kuwa amelaaniwa na amefukuzwa kutoka katik...
Imepokewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Sharti zenye haki...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa sharti bora kabisa kwa kutekelezwa ni zile zilizokuwa sababu ya uhalali wa kustarehe na mwana...
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Tahadharini sana na kuingia/kukaa kwa wanawake" Mtu mmoja katika Maanswari akasema: Ewe Mtume wa Allah vipi kuhusu shemeji? Akasema: "Shemeji ni kifo".
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amelaaniwa mwenye kumuingilia mke wake kinyume na maumbile".
Imepokewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu".
Imepokewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema".
Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kutazama ghafla, akaniamrisha nigeuze jicho langu.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alichinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kondoo wawili wazuri weupe wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akasema, Bismillahi Allaahu Akbar, na akaweka mguu wake ubavuni mwao.
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu".
Imesimuliwa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Abi Laila, kuwa, siku moja walikuwa kwa Hudhaifa, akaomba maji, Mmajusi mmoja akampa kitu cha kunywa, alipokiweka kikombe mkononi mwake, akakitupa, na akasema: Kwani si nilishamkataza zaidi ya mara moja au mbili - kana kwamba anasema: Sikufanya hivi kwa matashi yangu - bali nilimsikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera."
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".