/ Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekataza kunyoa kiduku

Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekataza kunyoa kiduku

Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekataza kunyoa kiduku.
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kunyoa baadhi ya nywele za kichwa na kuacha baadhi. Na katazo linawahusu watu wote, mwanaume mtoto mdogo na mkubwa pia, ama mwanamke hatakiwi kunyoa nywele za kichwa chake.

Hadeeth benefits

  1. Sheria ya Uislamu imetilia umuhimu wa muonekano wa kibinadamu.