- Katazo la kuingia kwa wanawake wa kando na kukaanao faragha, kwa ajili ya kuziba njia zinazopelekea kuingia katika uchafu.
- Katazo hilo ni kwa watu wa kando wote kwanzia kaka wa mume na ndugu zake wa karibu, ambao si haramu kwao kumuoa mwanamke, hivyo ni lazima kuchunguza ili kujua kama kuingia kwake kunapelekea kuwa faragha.
- Kujiweka mbali na maeneo yote ya kuteleza, kwa kuhofia kuingia katika shari.
- Amesema Imam Nawawi: Wamekubaliana wasomi wote wa Lugha ya kiarabu kuwa maana ya mashemeji ni ndugu wa karibu wa mume, kama baba yake na ami yake, na kaka yake, na mtoto wa kaka yake, na mtoto wa ami yake na mfano wao, nakuwa wakwe ni ndugu wa karibu wa mume, nakuwa wakwe wanakuwa kwa aina zote mbili.
- Ameufananisha ushemeji na kifo, amesema bin Hajari: Na waarabu hukifananisha kitu chenye kuchukiza na kifo, na namna ya kufanana kwake nikuwa ni kifo cha dini yakitokea maasi, na ni kifo cha mambo yote endapo yatatokea maasi kwani itakuwa wajibu kupigwa mawe, na ni kifo cha mwanamke kwa kuachana na mumewe endapo wivu utampelekea kumpa talaka.