- Inafaa kustarehe na vizuri vya Dunia alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake bila kupita kiasi au kujikweza.
- Himizo la kuchagua mke mwema; kwa sababu ni msaada kwa mume katika kumtii Mola wake Mlezi.
- Starehe bora ya Dunia ni ile itakayokuwa katika kumtii Allah au ikasaidia katika hilo.