- Sifa hii na ahadi hii ya adhabu ni maalumu kwa wanaume, ama wanawake, wanaondolewa katika hilo; kwa sababu wao wameamrishwa kusitiri mwili wao wote.
- Kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume huitwa kikoi; kama suruali, na nguo na vinginevyo, na vyote hivyo vinaingia katika hukumu ya kisheria iliyotajwa katika hadithi.