- Himizo la kuinamisha macho.
- Tahadhari ya kutazama kwa muda katika yale yaliyoharamishwa kuyatazama jicho linapodondokea ghafla na pasina kukusudia.
- Ndani ya hadithi kuna uharamu kwa kuwatazama wanawake, jambo ambalo waliishi nalo Maswahaba, kwa ushahidi wa kuwa Jariri radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa endapo litaangukia jicho lake katika kumtazama mwanamke pasina kukusudia, je hukumu yake itakuwa sawa na aliyekusudia kutazama?.
- Na pia inaonyesha namna sheria ilivyotilia maanani masilahi ya waja, kwa kuwaharamishia kuwatazama wanawake, kwakuwa swala hilo linaambatana na maovu ya dunia na Akhera.
- Kurejea Maswahaba kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kumuuliza katika yale yanayowatatiza, na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa watu wote kurejea kwa wanachuoni wao na kuwauliza katika yale yanayowatatiza.